loader
Picha

Hospitali yaanzisha huduma kwa mtandao

KUTOKANA na maambukzi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma ya ushauri wa daktari bingwa wa watoto kwa njia ya mtandao hususani video.

Utaratibu huo ulianza tangu jana na unawahusu wakazi wa Dar es Salaam pekee ambao wataweza kupata huduma hiyo ya kibingwa. Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, lengo la utaratibu huo mpya ni kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu.

Kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na maambukizi ya virusi vya corona, serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imekuwa ikiwasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo ya kitaalamu yanayotolewa na Wizara hiyo ili kujikinga na maambukizi hayo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, mpaka sasa kuna wagonjwa 20 wa covid-19 nchini.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

3 Comments

 • avatar
  Richard juma
  03/04/2020

  Comment watanzania tuna takiwa kira mmoja wetu kuzingatia taratibu zinazo torew na wataaramu wa afya%&

 • avatar
  Aron ngassa lutaja
  03/04/2020

  Comment

 • avatar
  Aroone ngassa lutaja
  03/04/2020

  Jaman watanzania tumuombe sana MUNGU Atupiganie kama alivyowapigania wana wa israel kuwatoa mikononi mwa farao kwa imani corona itapita lakini pia tufate maelekezo ya waaram na serikar kwa ujumla kama inavoagiza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi