loader
Picha

Abiria watakiwa kunawa kabla ya safari

SERIKALI mkoani hapa imeutaka uongozi wa Manispaa kuongeza nguvu ya kutoa elimu endelevu, usimamizi imara na kuhimiza matumizi ya kunawa mikono kwa sabuni.

Pia wasafiri na wahudumu katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu wametakiwa kunawa mikono kila mara hasa abiria kabla ya kuanza safari ili kujikinga na maambuziko ya virusi vya Corona (COVID-19).

Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuele Kalobelo ambapo alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Shailla Lukuba kusimamia maagizo hayo.

Kalobelo alitoa maagizo hayo alipotembelea Kituo cha Mabasi cha Msamvu jana akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo kuangalia utekelezaji wa hatua mbalimbali za kujikinga na janga la Corona.

Pia alimwagiza mkurugenzi huyo kuongeza watumishi wa afya katika kituo hicho cha mabasi cha Msamvu ili wafanye kazi kwa zamu na pia kuongeza askari mgambo watakaokuwa wakifuatilia utekelezaji wa maagizo ya serikali.

Katibu Tawala wa mkoa pia alimuagiza mkurugenzi huyo kuweka vipaza sauti ndani ya stendi hiyo kwa ajili ya elimu endelevu kwa wananchi na wasafri kutoka kwa wataalamu wa sekta ya afya kwa vile kituo hicho kina mwingiliano wa watu wengi wakiwemo wasafiri kutoka mikoa mbalimbali.

Pia aliwataka madereva wa mabasi kuhakikisha abiria wao wanapoingia na kushuka katika kituo hicho kikuu cha mabasi wanawawekeea vitakasa mikono mikononi mwao.

Katibu Tawala wa mkoa pia aliwashauri wananchi kupunguza msongamano usio wa lazima waliouzoea kuwasindikisha ndugu zao hadi ndani ya mabasi, badala yake waishie eneo la kusubiria wageni na wenye mizigo huduma hiyo itafanywa na wahudumu ndani ya stendi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa hiyo, Lukuba alisema timu ya wataalamu wa afya imekuwa ikifika mara kwa mara kutoa elimu kwa wananchi katika kituo kikuu hicho cha mabasi na pia kuna ofisa afya anayesimamia zoezi hilo kila siku.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mourice Masala ambaye pia ni msimamizi wa safari za mabasi ya Abood katika stendi hiyo, alisema mabasi yao kabla ya kufikishwa stendi kwa ajili ya kuchukua abiria yanakuwa tayari yamepuliziwa dawa

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi