loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuzingatie maelekezo tusiambukizwe corona

HATUA iliyochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Annamrngi Macha kwa wahudumu wa afya ni ya kuigwa katika wilaya zote nchini kwani kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa ugonjwa huu, kama ilivyo kwa magonjwa yote yanayoambukizwa na virusi, hauna tiba.

Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza kwamba kila mtumishi wa afya anayetoa huduma katika kliniki kwa wajawazito na watoto lazima aanze kwanza kwa kutoa elimu ya kuthibiti na kujikinga maambukizi ya virusi vya corona (Covid 19) katika vituo vyote vya afya na zahanati wilayani humo.

Juzi, mwandishi wa gazeti hili alishuhudia mkuu huyo wa wilaya akiwa kwenye vituo vya afya kutathimini utekelezaji wa agizo hilo alilotoa kwao.

Alitembelea vituo mbalimbali kuangalia kama elimu inatolewa na pia akakutana na watendaji wa kata, maofisa maendeleo ya jamii, maofisa afya na baadhi ya watoa huduma za afya. Hii yote ni kukazania kinga badala ya kusubiri kutibu ugonjwa.

Nasi kama chombo cha umma ambacho kinahamasisha utoaji wa elimu, tunampongeza kwa hatua hiyo.

Ni kutokana na juhudi zake hizo, pia tunawaomba viongozi wengine kuanzia ngazi ya mikoa, wilaya na vijiji kama ilivyo kitaifa, kuiga mfano wake.

Hata hivyo, tunatoa tahadhari kwamba, elimu inayotolewa itokane na maelekezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Kamati zilizoundwa kusimamia suala hili pamoja na Wizara ya Afya.

Tunaamini, kwenye vitongoji na vijiji, kwa maelekezo ya wakuu wa wilaya na mikoa, wataweka utaratibu kwa kila kituo cha afya na zahanati iwe ni binafsi au serikali, kabla ya kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wakiwemo wajawazito na watoto wanaokwenda kliniki, watapewa kwanza elimu ya kujikinga na maambukizi ya corona kabla ya huduma nyingine za kitabibu.

Pia kama ilivyo kwa Wilaya ya Kahama, ni vema kutengwe eneo maalumu kwa tahadhari katika vituo hivyo vya afya ili kama mtu anahisiwa, apumzishwe hapo kabla ya kuhamishiwa kwenye hospitali kubwa au maeneo yaliyobainishwa na waganga wakuu wa mikoa au wilaya.

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani, tayari kuna wagonjwa ambao kutokana ama kusafiri nje ya nchi au kukutana na aliyesafiri hasa katika nchi ambazo zimeathirika, inao wagonjwa 16 baada ya kupoteza mmoja na wengine watatu kupona kutoka jumla ya awali ya wagonjwa 20 hadi sasa.

Tunaishukuru Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kwa Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu ambaye bila kuchoka, amekuwa msitari wa mbele kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu hali ilivyo nchini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu jinsi jamii inavyoweza kujikinga na ugonjwa huu.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi