loader
Picha

Tuepuke taarifa zisizo sahihi janga la corona

TANGU kuingia nchini kwa mgonjwa wa kwanza aliyethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi wakielezea ugonjwa huo wengine wakipotosha aidha kwa kujua au kutokujua.

Taarifa hizo nyingine zimekuwa zikipitishwa katika mitandao ya kijamii, wengine wakipiga picha na vifaa visivyokidhi kutumika kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo, jambo ambalo linaweza kupunguza ari ya jamii kuona umuhimu wa kuchukua hatua.

Ni wazi kuwa serikali imetoa elimu mbalimbali kuhusu namna maambukizi ya ugonjwa huo, nini cha kufanya na hata yale yanayostahili kuepukwa, lengo likiwa ni kujiepusha katika kupata maambukizi ya virusi hivyo.

Ili kuepusha hali hiyo ya wananchi kuendelea kupeana elimu ambayo hawana uhakika nayo ni muhimu kwa wataalam wa afya nchini kutumia muda wao kwa kuelimisha jamii kwa kina kuhusu masuala mbalimbali kuhusu maambukizi hayo.

Katika hali hiyo, katika mitandao ya kijamii, wananchi wanashuhudia kuona matangazo mbalimbali ya vyakula vinavyotakiwa kuliwa kwa kipindi hiki ambapo maambukizi ya virus hivyo yapo nchini na wengine wakichanganya vyakula na majani na kuchemsha.

Wananchi wanashuhudia picha zinazoonesha mchanganyiko wa majani ya mwarobaini, yakichanganywa na tangawizi zikiwa hazijasangwa pamoja na ndimu ikionesha kuwa ndio kinga kwa maambukizi hayo.

Ni kweli kuwa linapotokea jambo, wapo wanaotumia mwanya huo kwa kudanyanya na wengine kwa kutokujua wakijikuta wakiendelea kupotosha jamii kuhusu suala hilo.

Ili jamii iwe na uelewa stahiki na kuchukua hatua zinazostahili ni vyema wataalamu wa afya kuona umuhimu wa kutoa elimu jambo litakalosaidia kujibu maswali kuhusu maambukizi ya virusi vya corona au pengine kutoa ushauri kwa kile kinachotakiwa kufanywa na manufaa yake.

Kwa mfano wapo wanaojua kwamba zipo sabuni maalumu zinazotakiwa kuoshea mikono na wengine wakiambiana kwamba aina fulani haiwezi kuosha inavyotakiwa na wengine wakidiriki kusema wapo baadhi wanaotumia jiki inayosafisha madoa kwenye nguo na kutumia kusafisha mikono.

Kadhalika wapo waliokwenda mbali wakidai kuwa hata vinywaji vikali vinafaa kusafisha mikono kwa madai kuwa hatua hiyo inaweza kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Baraza la Ushauri wa Watuamiaji wa Huduma za Mawasiliano Nchini ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi