loader
Picha

Corona yamchanganya Ndayiragije

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka nchini, Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema mlipuko wa virusi vya corona umewataabisha kwa sababu wameacha kazi na kukaa nyumbani.

Kabla ya kuenea kwa virusi vya corona nchini vilianzia China mwaka jana, Taifa Stars iliingia kambini kujiandaa na fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) iliyokuwa ifanyike mwezi huu, lakini michezo yote iliahirishwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ndayiragije alisema uwepo wa ugonjwa wa COVID 19 unaosababishwa na virusi vya corona imekuwa ni tatizo, kwani hawawezi kufanya chochote na wala hawajui utaisha lini.

“Kwa kweli ugonjwa huu umekuwa tatizo, kwanza tumwombe Mungu, kwa sababu tumeacha kazi na kukaa nyumbani. Sijui itaisha lini,”alisema kocha huyo wa zamani wa Mbao, KMC na Azam FC.

Alisema mpaka sasa hakuna anayejua itakuwaje baadaye wala michezo itarudishwa lini zaidi ya kuomba ugonjwa upite mbali ili warudi salama na kusisitiza afya ndio muhimu kwanza.

Si tu kwa upande wa Afrika, bali tatizo hilo linalosumbua duniani kote limesababisha michezo kadhaa mikubwa kufutwa na mingine kusogezwa mbele kuzuia kuenea zaidi.

Stars ilivunja kambi na wachezaji wote kurudi nyumbani baada ya Serikali kutangaza kusitisha michezo na mikusanyiko kwa kipindi cha siku 30 hadi pale hali ya ugonjwa huo uliosambaa mataifa mbalimbali utakapotangazwa kupungua au kumalizika.

Ndayiragije aliiongoza Stars kufuzu fainali hizo za Chan mwaka jana na mara ya mwisho kufuzu ilikuwa mwaka 2009 na kuirudisha Tanzania katika ramani ya soka la kimataifa.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi