loader
Picha

Fifa kuongeza umri michezo Olimpiki

SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka, Fifa, linajiandaa kuongeza umri katika mashindano ya soka ya wanaume ya Olimpiki yatakayofanyika mwakani jijini Tokyo hadi miaka 24 badala ya 23 ya sasa.

Shirikisho hilo linalohusika na soka limependekeza wachezaji wa umri huo ndio wacheze katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo iliyopangwa kufanyika mwaka huu kabla ya kuahirishwa hadi mwakani kutoka na mlipuko wa virusi vya corona.

Wachezaji waliozaliwa kuanzia au baada ya Januari 1, 1997 wataruhusiwa kucheza michezo hiyo.

Lakini bado haitathibitishwa rasmi na mamlaka husika ya Fifa. Mashindano hayo yanatarajia kuanza kabla ya sherehe za ufunguzi rasmi zilizopangwa kufanyika Julai 23, 2021.

Bado utaratibu wa kutumia wachezaji watatu waliozidi umri utaendelea kutumika katika kila nchi.

Mashindano ya wanawake ya mwakani yenyewe hayana kiwango cha umri.

Wakati huohuo, Fifa imeamua kufutilia mbali mashindano yote ya wanaume na wanawake, ambayo yalipangwa kufanyika kuanzia Juni 2020 kutokana na virusi hivyo corona.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: ZURICH, Uswisi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi