loader
Picha

Judo wafurahia kusogezwa Olimpiki

CHAMA cha Judo kimesema kusogezwa kwa Michezo ya Olimpiki kumetoa fursa ya wao kujipanga kwa muda mrefu kutafuta michezo ya kufuzu kwa ajili ya mwakani.

Michezo ya Olimpiki iliyokuwa ifanyike Julai mwaka huu Tokyo Japan, imesogezwa mbele hadi mwakani kutokana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa corona vinavyoenea kwa kasi duniani.

Akizungumza na gazeti hili jana Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Innocent Mallya alisema wanahitaji kujipanga upya na hasa baada ya kupungua kwa virusi vya corona kwa kuangalia nini wafanye kupata michuano ya kimataifa.

“Kwa sasa hatuna cha kufanya tunasubiri mlipuko wa corona uishe tujipange upya kwa mashindano mbalimbali yajayo ikiwemo Olimpiki, kwasababu wameahirisha hivyo, hatuna budi kuja na mikakati mingine ya mwakani,” alisema.

Wakati wanafikiria nini cha kufanya kupata mashindano ya kufuzu, alitoa tahadhari kwa wachezaji wake kuwa makini kujiepusha na mikusanyiko itakayowaingiza kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

Mallya alisema kama ni mazoezi waendelee kufanya wakiwa nyumbani kujiimarisha zaidi kiafya. Judo ni miongoni mwa michezo ya Tanzania inayopewa nafasi ya kushiriki Michezo hiyo ya Olimpiki endapo wachezaji wake watafuzu kwa michezo hiyo.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi