loader
Picha

Msangi: Mwakinyo atarudi 10 bora

PROMOTA wa ngumi za kulipwa, Jay Msangi amesema wana mkakati wa kuhakikisha bondia wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo anarudi katika kiwango na kushika 10 bora.

Msangi aliliambia gazeti hili kuwa Mwakinyo licha ya kuporomoka kwenye viwango vya ubora wa dunia, lazima akacheze pambano lake la Ujerumani baada ya kuisha kwa virusi vya corona na akishinda atarudi katika kiwango chake.

Mwakinyo alitarajiwa kwenda kupambana na Mjerumani, Jack Culcay kuwania ubingwa wa dunia wa WBO Machi 21, lakini mlipuko wa virusi vya corona uliharibu mipango hiyo na kuahirishwa.

“Kama Mwakinyo angekwenda Ujerumani na kumpiga Culcay ina maana kuwa angepanda zaidi, lakini kuahirishwa kwa pambano hilo kumeharibu mipango,”alisema.

Kutokana na viwango vya dunia vilivyotolewa na mtandao wa kazidata wa BoxRec Msangi alisema kuahirishwa kwa pambano hilo kunatoa fursa kwa bondia huyo kujipanga vizuri na kurudisha heshima yake baadaye.

Alisema ana imani atarudi kwenye ubora kinachohitajika ni bondia kuendelea na mazoezi yake binafsi hadi pale matatizo ya ugonjwa yatakapoisha ili kwenda kutengeneza historia nyingine itakayompandisha juu.

“Tuna imani tukienda Ujerumani lazima tumpige Culcay na mipango inaendelea hatujakata tamaa,”alisema Msangi. Mwakinyo ameporomoka hadi katika nafasi ya 86 kutoka nafasi ya 18 kwa ubora katika mchezo wa ndondi duniani.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi