loader
Picha

Ataja sababu Tanzania kuboronga riadha

TANZANIA itaendelea kutofanya vizuri katika mashindano ya riadha kutokana na kutokuwa na wataalam wa mchezo huo.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Riadha Tanzania (RT) na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Hamad Ndee katika mahojiano maalum na habari Leo juzi kuhusu maendeleo mazima ya mchezo huo, ambao Tanzania ilitamba huko nyuma.

Dk Ndee ambaye pia ni mwanariadha wazamani wa kimataifa wa Tanzania alisema kuwa tatizo kubwa la Tanzania kutofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ni sababu ya kutokuwa na wataalum waliopata mafunzo ya mchezo huo.

Ndee ambaye wakati wa ukimbiaji wake aliwahi kushiriki Michezo ya Afrika, Jumuiya ya Madola na hata Olimpiki kwa nyakati tofauti, alisisitiza kuwa wengi wa walimu wa riadha ni wasimamizi wa mazoezi tu na hawana ujuzi wa kufundisha mbinu za mchezo huo.

Alisema hata hizo mbio ndefu (marathoni), ambazo watu wengi wanafikiri kuwa Tanzania inafanya vizuri, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa, “hatufanyi vizuri kutokana na kutokuwa na watalaamu.”

Alisema kuwa amekuwa akiandika maandiko mbalimbali ili kupata fedha kutoka Riadha ya Dunia (WA) kwa ajili ya kuwafundisha walimu wa walimu, ambao wangeenda kuwafundisha wanafunzi mashuleni, pamoja na kupata fedha hizo, lakini zoezi hilo halikufanikiwa.

Alisema kuwa uongozi wa RT umekuwa ukimuangusha kwa kushindwa kutumia fedha hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa na badala yake zimepelekwa katika matumizi mengine kabisa, na kushindwa kuwafundisha walimu wa walimu na watalaamu wengine.

Akifafanua zaidi, Dk Ndee alisema kuwa, mfano aliandika WA andiko la kuiombea RT Dola za Marekani 100,000 (sawa na Sh milioni 231.4) kwa miaka minne, ambapo kila mwaka walitakiwa kutumia Dola 25,000 (sawa na Sh milioni 58), ambazo unapewa mwaka unafuata baada ya kutolea maelezo ya matumizi ya mwaka uliopita, fedha hizo zilitumika kwa matumizi mengine.

Alisema fedha hizo za miaka kwa ajili ya mafunzo ya riadha kwa miaka minne zilianza kuletwa mwaka 2016 hadi mwaka 2019 na anamshukuru Mungu, RT ilipata fedha hizo kwa kipindi chote baada ya yeye mwenyewe (Ndee) kuziandikia maandiko kila mwaka, jinsi fedha hizo zilivyotumika, lakini hakupewa kuwaendeleza walimu wa walimu wa riadha.

Katika miaka ya nyuma, Tanzania ilikuwa ikifanya vizuri katika michezo mbalimbali ikiwemo ile ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki na Afrika baada ya wanariadha wake kurudi na medali kutoka katika michezo hiyo, lakini miaka ya karibu imekuwa msindikizaji tu.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi