loader
Picha

Tevez ataka wanasoka wajitoe zaidi

MCHEZAJI soka wa Argentina, Carlos Tevez amesema soka lazima lifanye zaidi kusaidia jamii hasa sekta zile za majanga na kuwataka wachezaji wenzake kuwaangalia zaidi wale wenye matatizo badala ya kujijali wenyewe.

Tevez, ambaye yuko katika miezi ya mwisho ya mkataba wake na Boca Juniors, aliwaombwa wachezaji wenzake kutoa sehemu ya mishahara yao, lakini akisema kuwa wachezaji wakubwa wana fedha nyingi na wanatakiwa kuwasaidia wengine.

“Wacheza soka wana uwezo wa kukaa miezi sita, au mwaka na zaidi (bila ya kulipwa kitu lakini wakaishi vizuri tu), “alisema Tevez juzi katika mahojiano na America TV ya Argentina. “Inabidi kushukuru sana kuwa tuko salama na tunaongea. Inatubidi sisi tuvae uhusika wao.”

Tevez, ambaye alichezea klabu za Manchester (United na City) pamoja na Corinthians, West Ham na Juventus, alisema ana matumaini janga la mlipuko wa corona litawalazimisha watu kubadili tabia.

“Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa kitu kimoja na kujaribu kusaidia watu wenye mahitaji zaidi, “alisema. “Natumaini dunia inaonesha mshikamano wa hali ya juu. Wote tuko sawa. Corona imetupiga sote kwa njia ile ile, mababu na mabibi imewaathiri zaidi, wawe Argentina au Marekani.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: BUENOS AIRES, Argentina

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi