loader
Picha

Muumini- Ni rahisi kukutana JPM kuliko Diamond

MWIMBAJI wa muziki wa dansi, Muumini Mwijuma amesema ni vigumu kuonana na msanii Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Akizungumza jana Muumin alisema mara ya mwisho kuonana na Diamond ilikuwa 2010 Temeke, Dar es Salaam lakini alipata shinda hadi kuonana na kuzungumza naye.

“Kuna wakati nilipiga simu akapokea mama yake akanimbia kama una shida na Diamond ongea na mimi. Nilijisikia unyonge kwa sababu yeye sio msanii mwenzangu, nilitaka nizungumze na mwanamuziki mwenzangu,” alisema.

“Natamani kufanya naye kazi lakini toka siku hiyo sijawahi kuonana naye tena, hata ukiwaambia wale watu wake, ni rahisi kukutana na Rais Magufuli kuliko kukutana na Diamond,” aliongeza Muumini.

Machi 6 mwaka huu Muumini alitangaza kurejea kwenye muziki akiwa na bendi ya Shadai na kutoa wimbo unaoitwa Nimefulia, ambayo anatarajia kuizindua wakati wowote baada ya kumalizika kwa janga la corona.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi