loader
Picha

Masanja ajisalimisha kwa DC

Msanii wa vichekesho Emmanuel Mgaya, ‘Masanja Mkandamizaji’ amejisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi kuitikia wito aliotoa juzi baada ya kuhoji watu kwa utani kuhusu virusi vya corona vinavyoeneza ugonjwa wa COVID 19.

Juzi Katambi alimtaka Masanja ajisalimishe ofisini kwake au polisi kwa mahojiano baada ya kuwahoji watu kwa utani kuhusu virusi vya corona katika jiji la Dodoma.

Katambi amesema ugonjwa huo umekuwa tishio ulimwenguni na anashangaa kwa nini Masanja kaamua kufanya utani, hivyo wanataka kujua nini hasa lengo lake.

Katika kipande cha video kinachosambaa mtandaoni Masanja anaonekana akiwauliza wakazi wa Dodoma wanahitaji kuletewa COVID-19 ngapi katika jiji lao.

Baada ya Masanja kufika katika ofisini kwa Katambi jana alikutana na kamati nzima ya ulinzi na usalama ya wilaya na kueleza kuwa kipindi chake yeye anarusha maudhui ya watu wanaokosea tu.

“Kipindi changu mimi nanarusha maudhui yaliyokosewa mtu akijibu sahihi hiyo situmii hivyo nitaka kuonesha kuwa bado kuna watu ambao hawaelewi maana ya ugonjwa wa COVID 19,” amesema Masanja.

Pia Masanja aliwataka watu wote kuungana na serikali katika kutokomeza virusi vya corona kwani ni janga.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi