loader
Picha

Anko Zumo: Nitamlea Mai katika maadili

MWIGIZAJI Anko Zumo amekiri umaarufu wa mtoto wake, Maisara Zumo ‘Mai’ ambaye pia ni mwigizaji unaweza ukampa taabu kwenye malezi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Anko Zumo alisema umaarufu kwa watoto wengi kwenye tasnia ya uigizaji huleta madhara kwenye maadili, lakini yeye atajitahidi kumlea vizuri mtoto wake.

“Ukiangalia waigizaji waliokuwa maarufu tangu wadogo, lazima kuna kitu walikuja kukosea, hata kama walipatia sana suala la maadili linakuwa shida unakuta uvaaji wao hauko sawa,” alisema.

Pia alisema licha ya Mai kuwa maarufu kuliko wao wanajitahidi kuhakikisha wanafanya kazi ili kujitengenezea jina nje ya mtoto wao.

Anko Zumo na mke wake na mtoto wao Mai ni waigizaji wa vichekesho kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram na Yutube, lakini Mai amekuwa akifanya kazi na waigizaji wakubwa kama Jacquiline Wolper, Gabo, Riyama na wengine wengi na kufanya vizuri.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi