loader
Picha

11 wadakwa mpakani wakikwepa karantini

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya Tanzania na Kenya wakitumia njia za panya kuvuka katika vijiji vya ujirani mwema vya nchi hizo wakijaribu kukwepa taratibu za kudhibiti kuenea maambukizi ya virusi vya corona.

Mratibu wa Kituo cha Uhamiaji cha Horohoro, Singwa Mokiwa alisema wamefanikiwa kukamata watu hao baada ya kuweka vizuizi maalumu katika njia za panya zinazotumiwa na watu kuvuka katika kijiji cha Horohoro na Jasini usiku wa kuamkia juzi.

Mokiwa alisema baada ya kuweka utaratibu maalumu kwenye eneo huru katika mpaka huo wa kuwapima wale wote wanaopita ili kubaini dalili za ugonjwa huo, baadhi ya watu wanaona ni usumbufu na kuamua kutumia njia za panya.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Horohoro, Lekule Ole Lengai alisema watu wengi wanajaribu kutumia njia hizo za panya kwa ajili ya kukwepa kuwekwa karantini.

“Unajua hadi hivi sasa tayari kuna watu zaidi ya 20 wamewekwa karantini baada ya kuvuka kihalali kwenye mpaka, baada ya kuona hivyo wengi wameingiwa na woga na kuamua kutumia njia hizo za panya hasa muda wa usiku,”alisema Lengai.

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeweka mkakati wa upatikanaji wa ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Horohoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi