loader
Picha

'Wazazi lindeni watoto wasifanyiwe ukatili'

WAZAZI na walezi wametakiwa wakati huu wa shule kufungwa kutokana na janga la corona, kuhakikisha wanawalinda watoto wawapo nyumbani kwa sababu asilimia 60 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hufanywa nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana, Lilian Liundi, watoto wa kike wapo katika hatari ya kupata mimba za utotoni na kufanyiwa aina nyingine za ukatili wa kijinsia iwapo hatua hazitachukuliwa.

Katika taarifa hiyo ya Lilian, inaonesha kuwa takribani asilimia 60, ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hutokea majumbani, na wanaofanya vitendo hivyo ni aidha ndugu wa karibu au majirani.

Kutokana na mazingira hayo, Lilian aliwataka wazazi na walezi kwa wakati huu ambao wapo nyumbani na hivyo kuwataka wazazi kuchukua hatua madhubuti kuwalinda.

“Watoto wanabaki nyumbani na wazazi wao wanakwenda kazini. Katika hali hii unyanyasaji wa kingono unaweza kujitokeza na kusababisha mimba za utotoni. Wazazi tuwe makini sana kwa hili,” alisema Lilian.

“Kwa ujumla, ukatili wa kijinsia huongezeka wakati wa majanga kama haya, si tu kwa watoto bali pia kwa wanawake,” alisema Lilian.

Lilian katika taarifa yake alisema ni muhimu kwa sasa kuweka mikakati madhubuti ya kuwalinda kwa kuwafikia, na kuwapelekea huduma na elimu sahihi huko waliko ili waweze kujikinga.

Akizungumzia huduma za kliniki kwa wajawazito na watoto, ambapo mara nyingi huwa na msongamao wa watu alisema ni vyema taratibu za kujikinga ikiwemo kunawa mikono, kupata huduma kwa kukaa mbali kwa mita moja kutoka mtu na mtu, huku wakijipanga kwa foleni kuangaliwa.

“Kwa upande wa afya ya uzazi ya mama na mtoto, ukweli wakitabibu kuhusu mwanamke mwenye ujauzito na aliyetoka kujifungua ni kuwa, kinga zake si imara hususani kwa kipindi anaponyonyesha.

“Kwa hospitali zilizo na wauguzi wanawake, wazazi wa chini ya mwaka mmoja, tunashauri kuwa wasipangiwe majukumu ya kuhudumia wagonjwa wa corona,” alisema Lilian.

Lilian aliwataka wazazi wote, baba na mama kuhakikisha kuwa wanawajibika kujikinga wanapokuwa katika shughuli zao zinazowalazimu kutoka nyumbani kwa sababu ikitokea mzazi ameambukizwa akirudi nyumbani ataweza kuwaambukiza watoto, na hivyo juhudi ya sekikali kuwalinda watoto haitokuwa na maana.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi