loader
Picha

Kocha- Kuna wachezaji hawastahili kucheza Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga Luc Eymael, ametangaza hali ya hatari kwa wachezaji wavivu na wasiojituma , akidai msimu ujao hawatokuwa na nafasi kwenye kikosi chake, huku akiainisha kuhitaji wachezaji wapya nane msimu ujao.

Yanga tayari imeanza mazungumzo na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao inaelekea ukingoni na tayari imemuongezea mkataba nyota wake raia wa Ghana, Bernard Morrison.

Eymael amezungumza na gazeti hili na kueleza kuwa mipango yake ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkuwa utakaoifikisha Yanga kule anakotaka yeye na mashabiki wa klabu na kwamba anahitaji wachezaji wapya nane ili kuboresha kikosi chake na kati ya hao wanne ni wachezaji kutoka nje na wanne ni Watanzania.

“Niko hapa kwa miezi mitatu, nimebaini Yanga ni timu kubwa, lakini ina wachezaji wasiyostahili kuichezea, ndio maana nimeamua kuja na mkakati huu ili kuhakikisha timu inarudi kwenye mafanikio,” alisema Eymael.

Mbelgiji huyo alisema anataka kujenga timu ya mfano itakayopambana na timu yoyote ndani na nje ya nchi na kupata matokeo na hilo linawezekana na kwamba akikamilisha hayo anayoyataka, basi mashabiki wao wasubiri makombe kwani anaamini hakuna timu itakayowasumbua.

“Akili za mashabiki na wachezaji wengi wa Tanzania ni kushinda mechi ya wapinzani, kitu ambacho siyo, kushinda mechi ya watani ni jambo zuri, lakini unapata pointi tatu kama ambavyo ungeifunga timu nyingine, sasa nataka kujenga timu ambayo kila mechi itakuwa muhimu na siyo mechi ya Simba tu,” alisema.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi