loader
Picha

Gadiel- Nakaa benchi lakini nainjoi

BEKI wa kushoto wa Simba, Gadiel Micheal, amesema pamoja na kukaa benchi muda mwingi kwenye timu hiyo, lakini anafurahia maisha ya Msimbazi.

Gadiel ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo kwenye kikosi cha watani zao Yanga, lakini tangu alipojiunga na Simba mwanzoni mwa msimu amekumbana na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa Mohamed Husseni ‘Tshabalala’.

Akizungumza na gazeti hili, Gadiel alisema changamoto aliyokutana nayo ni ya kawaida kwake na ndiyo kwanza inamuongezea ari ya kujituma ili aweze kumshawishi kocha Sven Vandenbroeck kumpa nafasi.

“Kukaa benchi ni vitu vya kawaida kwenye mpira, na vinatumika kumpa mtu ari ya kupambana ili kurudisha kiwango chake, lakini benchi halinifanyi kujutia kuondoka Yanga, ukweli kwamba nafurahia maisha ya Simba,” alisema Gadiel.

Beki huyo alisema kupanda au kushuka kwa kiwango ni jambo la kawaida kwa mchezaji yeyote, hivyo halimpi hofu sana kwa kuwa anaamini ni upepo mbaya ndio ambao umempitia na kufanya ashuke kiwango.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi