loader
Picha

Msikie Humud ana jambo lake

SI unafahamu kuwa kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humud ameonesha kiwango cha juu mno msimu huu kiasi cha kugeuka lulu na kuhusishwa kuhamia katika timu mbalimbali? Sasa mwenyewe amefunguka kuhusiana na anachowaza kwa sasa.

Si siri kwamba kumekuwa na asilimia kubwa za mchezaji huyo wa zamani wa Simba msimu ujao kwenda kukipiga Yanga ikielezwa kuwa benchi la ufundi la timu hiyo limevutiwa na huduma yake na kinachosubiriwa ni kukamilika kwa baadhi ya vitu.

Hata hivyo, Humud ambaye ameeleza kwa sasa si muda sahihi kulizungumzia hilo lakini amekiri kuwa huu ni wakati wake wa kurejea upya kwenye ramani na anapambana kuhakikisha hilo halifutiki licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi zinazoweza kupelekea kubadilika kwa mambo mara baada ya kurejea kwa Ligi Kuu.

Ni hivi, ligi pamoja na sehemu za kufanyia mazoezi zimesimamishwa kutokana na tishio la virusi vya ugonjwa wa corona, kitu ambacho kinamuumiza kichwa Humud nini cha kufanya ili aendelee kusalia kwenye kiwango chake ili ligi ikirejea aendelee pale alipoishia na asishuke thamani aliyonayo sasa ili atimize ndoto zake.

“Kivyovyote inakuwa haingii akilini kwa mchezaji ambaye amefanya makubwa msimu mzima na kisha kuporomoka kwenye mechi chache zilizosalia mara baada ya ligi kurudi, hivyo ni lazima kutafuta nini cha kufanya muda huu ili nimalizie vizuri pale nilipoishia na ndotozangu nilizokuwa nazo mara baada ya kuisha kwa msimu zitimie.

“Ligi iliposimama nilikuwa najumuika na watu wenye uzoefu wa soka na mazoezi ili nisipungue sana pale nilipoishia lakini sasa hadi sehemu hizo pia zimesimamishwa kwa sasa, kwa hiyo nipo kwenye kutafuta nini cha kufanya zaidi ili nikae sawa na nisipoteze hii nafasi kama ligi itarejea mapema baada ya kuisha kwa ugonjwa huu uliopo.

“Kama mchezaji mwenye malengo, hii ni nafasi yangu kubwa na hakuna siri katika hilo. Nimepambana vya kutosha na siko tayari kupoteza katika mechi hizi chache zilizosalia, hii ni nafasi yangu ya kumaliza kama nilivyoanza ili ninayoyafikiria yaende kama yalivyo,” alisema Humud.

Licha ya Mtibwa kutofanya vizuri msimu huu katika ligi lakini Humud amekuwa akitakata katika sehemu ya kiungo ya timu hiyo ya Morogoro na kuisaidia kunyanyua ndoo ya Kombe la Mapinduzi kwa kuitoa Yanga katika nusu fainali kabla ya kuibamiza Simba kwenye mchezo wa fainali kwa ushindi wa bao 1-0.

Imeelezwa kuwa licha ya kocha wa Yanga, Luc Eymael kwenye faili lake kuwa na majina ya viungo kadhaa anaowahitaji msimu ujao lakini Humud pia ni sehemu ya mahitaji hayo.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi