loader
Picha

Coastal haijafikiria kumuuza Bakari Nondo

WAKATI Simba ikijipanga kumvuta beki wa kati wa Coastal Union, Bakari Nondo katika kikosi chao, taarifa kutoka ndani ya Coastal zimeleta ukakasi katika kukamilika kwa dili hilo.

Iko wazi kuwa Nondo amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu kiasi cha kuwa beki tegemeo wa kikosi cha Taifa Stars na kupelekea Wekundu hao kutupa ndoano ya kunasa saini ya mchezaji huyo anayetajwa kuwa na mkataba na Coastal Union mpaka mwaka 2021.

Sasa taarifa hizo zimemfikia Mwenyekiti wa Coastal, Steven Mnguto ambaye bila ya kung’ata maneno ameeleza kuwa hawako tayari kumuachia beki huyo kwa sasa ndiyo maana wanashindwa hata kutaja thamani ya dau la mchezaji huyo.

Mguto alifafanua zaidi kuwa kama timu bado wanahitaji kuendelea kuonesha uwezo ambapo angalau msimu huu wameonekana kukaa sawa, hivyo kuhusu kuuza wachezaji hawajalifikiria hilo kwa sasa hasa kwa beki wao huyo kisiki anayezitoa udenda timu nyingi za Ligi Kuu Bara hulu taarifa nyingine zikichagiza kuwa Nondo yupo kwenye mipango ya kwenda kulipiga nie ya nchi mara baada ya kumaliza kandarasi yake Coastal.

“Si kwamba tumekaa katika njia ya mchezaji yaani yeye anahitaji kupiga hatua kisha sisi tukamzuia isipokuwa kama timu hatujafikiria kumuuza Nondo kwa sasa. Ni mchezaji wetu na yupo ndani ya mafanikio yetu madogo ya msimu huu.

“Taarifa za kutakiwa tumezisikia kama ilivyo kawaida ya wachezaji na uhalisia wa mchezo wa soka wenyewe kwamba unapofanya vizuri basi watu wanakuona na timu zinahitaji kuwa na wewe lakini sisi kama uongozi bado hatujafikiria kumuuza beki wetu, tunaihitaji zaidi huduma yake katika kuikuza timu lakini kama kutakuwa na mengine nafikiri hayo ni baadaye,” alisema Mnguto.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi