loader
Picha

Mashine kutafsiri kazi za ubongo

WANASAYANSI wameweza kuongeza utaalamu zaidi wa kutambua jinsi binadamu anavyozungumza kwa kuangalia mfumo wa ubongo wake.

Wataalamu hao wameweza kuhamisha mfumo wa ubongo kwa jinsi sentensi zinavyoundwa katika uhalisia na kupata kiwango cha makosa cha asilimia tatu katika neno.

Awali mashine ya ubongo ilikuwa ina uwezo mdogo wa kutambua vitu kwa namna hiyo. Utafiti huo ulichapishwa katika Jarida la 'Nature Neuroscience'.

Awali mfumo huo wa ubongo ulikuwa unatambua maneno ambayo yanayoongelewa kwa asilimia ndogo ya maneno.

Mtaalamu wa kusoma mashine hiyo ya ubongo, Dk Joseph Makin kutoka Chuo Kikuu cha California, San Francisco (UCSF), amesema Marekani wamejaribu kuboresha kuhakikisha kuwa inasoma ipasavyo.

Watu wanne waliojitolea waliweza kusoma sentensi wakati mashine hiyo ikisoma shughuli ambazo ubongo unafanya. Shughuli za ubongo zinaweza kuwa katika mfumo wa komputa, ambapo unaweza kuwasilisha maelezo ya takwimu fulani.

Sifa ambazo zinaweza kufanya ubongo kufikia kusoma sentensi huwa inategemea muundo wa sentensi kuanzia kwenye herufi na maelekezo ya matamshi kama ni swali au amri? Namna nyingine inayofanya mashine hiyo itambue neno kwa neno mpaka sentensi inapoundwa ni idadi ya sentensi.

Mfano hotuba inaweza kunakiliwa katika mfumo huo kuanzia sentensi 30 hadi 50. Watafiti wamesema kuwa bado wanafanya utafiti zaidi ili kutambua pia kama mfumo huo unaweza kutambua lugha tofauti na Kiingereza.

Lakini waliongeza kuwa mashine hiyo, haitambui sentensi kwa namna ilivyoundwa. Wamelitambua hili kwa kadri walivyojaribu kuongeza sentensi.

Wanasayansi wanasema kuwa mashine inaweza kutambua neno moja na sio sentensi. Hiyo inamaanisha kuwa kuna uwezekano wa sentensi kutotambuliwa wakati wa mafunzo yao.

Wakati mfumo wa komputa ulipopewa mafunzo ya jinsi ubongo unavyofanya kazi na maneno ya mtu kabla ya mafunzo, matokeo yake yanaonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa na vyema teknolojia hiyo ikatumike kwa watu wengine.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: CALIFORNIA, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi