loader
Picha

Tanasha: Sitaki mwanangu akose mapenzi ya baba

BAADA ya Tanasha Donna kuachana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, amesema atahakikisha mtoto wake anapata mapenzi yote kutoka kwa baba yake.

Akizungumza na mtandao wa ‘True Love Magazine’ uliopo Kenya, Tanasha alisema anashirikiana na Diamond kwa karibu kuhakikisha mtoto wao anapata huduma zote na mapenzi ya pande zote mbili ili mtoto wao akue kwenye misingi stahili.

“Kwa upande mwingine nimepoteza kitu kikubwa, mtoto amehusika, nafikiria kuhusu mtoto wangu sio mimi, sitaki mwanangu akue bila mapenzi ya baba, napigana kuhakikisha hilo linatimia,” amesema Tanasha.

Baada ya kuachana na Diamond, Tanasha aliacha gari aina ya Toyota Land Cruiser aliyopewa kama zawadi ya siku ya kuzaliwa na Diamond nchini Tanzania kwa kuwa anayo magari mengine kwao.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi