loader
Picha

'Ben Pol akinioa nitazaa watoto wengi'

MPENZI wa msanii, Bernad Paul ‘Ben Pol’, Anerlisa Muigai, amesema anaweza kuzaa baada ya kufunga ndoa na si vinginevyo.

Ben Pol na Anerlisa waliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi mwishoni mwa mwaka 2018 na kila mmoja ameonekana kumuunga mkono mwenzake katika masuala ya maendeleo.

Anerlisa alisema hayo alipoulizwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na shabiki aliyetaka kujua uwezekano wa kupata mtoto na msanii huyo na kujibu kama ifuatavyo.

“Nafikiri akinioa nitakuwa na watoto wengi sana kwa sababu napenda watoto zaidi ya hapo siwezi kuongeza jambo lingine.”

Katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mtoto wa Ben Pol iliyofanyika wiki tatu zilizopita, Anerlisa alimhakikishia Ben Pol atamlea mtoto wake vizuri na kumpa upendo kama mama yake mzazi.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi