loader
Picha

Mrembo aachwa kisa 'Bedroom'

MREMBO, Nicole Joyce Berry, ambaye ameonekana kwenye video ya wimbo wa ‘Bedroom’ wa Rajab Abdul ‘Hermonize’, amedai kuachwa na mpenzi wake kwa sababu ya kujiachia sana katika video hiyo.

Akizungumza na kipindi cha e-Newz cha EAT, alisema baada ya mpenzi wake kuona video hiyo aliamua kuchukua maamuzi hayo na sasa yupo peke yake.

“Najuana na Harmonize kabla ya video hii, wala haijaniletea madhara makubwa japo nilikuwa na mwanaume wangu lakini baada ya kuona akaniacha, sasa hivi sina tena mpenzi,” alisema Nicole.

Baada ya video hiyo pia Harmonize alikiri mrembo huyo alitikisa ndoa yake na Sarah lakini akawa mvumilivu hadi kumaliza kutengeneza video hiyo ambayo hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi