loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bakwata yaagiza msikiti wa Ngazija ufunguliwe

Bakwata yaagiza msikiti wa Ngazija ufunguliwe

SIKU tatu baada ya Msikiti wa Ngazija katika Jiji la Dar es Salaam, kufunga shughuli zake kwa siku 30, Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limetaka ufungue shughuli hizo.

Msikiti huo ulifunga shughuli zake kuanzia Machi 30 hadi Aprili 19, mwaka huu kujikinga na corona.

Hata hivyo, katika taarifa ya uongozi wa msikiti huo iliyotolewa siku tatu baada ya kuchukuliwa kwa uamuzi huo, sasa umefunguliwa baada ya kikao na Baraza la Mashehe la Mkoa wa Dar es Salaam.

“Na kwa maslahi mapana tumeonelea tufungue msikiti wa Ngazija kuanzia Aprili 3, mwaka huu, wakati tukiendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya msikiti katika kujilinda na maambukizi haya ya maradhi ya Covid-19,” ilisema taarifa ya uongozi wa msikiti huo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa msikiti huo, utakuwa unaangalia pia mwitikio wa waumini katika kufuata maelekezo ya njia za kufuata salama za kuingia na kutoka msikitini.

Akizungumza kuhusu uamuzi wa Bakwata wa kuufungua msikiti huo, Msemaji wa Bakwata, Said Mpeta alikiri msikiti huo umefunguliwa baada ya kujiridhisha tahadhari za kujikinga zinaweza kuchukuliwa.

“Ni kweli ulifungwa ili ujiweke sawa kwenye ulinzi huo wa maambukizi ya corona, lakini sasa tayari huduma muhimu zinatolewa ikiwa ni pamoja na kutoa tahadhari za kufuatwa kila anayeswali,” alisema Mpeta.

Alitaja baadhi ya tahadhari zilizochukuliwa kuwa ni kuwekwa kwa maji na sabuni za kunawa, lakini kila muumini kutakiwa kukaa kwa umbali maalumu baina yake na muumini mwenzake.

Machi 29, mwaka huu uongozi wa msikiti huo uliufunga baada ya kutathmini hatua zilizochukuliwa mwanzoni na kutafakari hatari za mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 na mkusanyiko wa waumin wakati wa sala.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/00c423a0181ec81d4e25324ad0155481.jpeg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi