loader
Picha

Diamond ahusishwa Mawenzi Market

MSANII wa muziki wa Bongo fl eva, Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amehusishwa kutaka kuinunua timu ya Mawenzi Market FC ya mkoani, Morogoro inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Hivi karibuni uongozi wa timu hiyo ulitangaza kuuzwa timu hiyo kwa Sh milioni 100 kutokana na ukata unaoikabili. Taarifa za ndani zinasema huenda Diamond akainunua timu hiyo na kuibadilisha jina na kuiita Wasafi FC.

Ikumbukwe kuwa Januari mwaka huu akifanya mahojiano katika kipindi cha Sports Arena kinachorushwa na kituo cha Wasafi FM, Diamond alisema anataka kuanzisha kituo cha kukuza vipaji akishirikiana na Samuel Eto’o na Didier Drogba. Pia alisema ataanzisha klabu ya Wasafi FC ambayo atahakikisha inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza gazeti Katibu wa Mawenzi Market, Juma Kilangilo alisema wadau wengi wameonesha nia ya kuinunua timu hiyo lakini ni mapema kuwataja kwa sababu hawajafikia makubaliano ya mwisho.

Alipoulizwa endapo Diamond amezungumza nao kuhusu kuinunua timu hiyo, alikiri kusikia habari hizo na kusema kama ni kweli itakuwa jambo la heri na kuwakaribisha wote wenye nia ya kuinunua timu hiyo kufika ofisini kwao.

Mawenzi Market inashika nafasi ya nane kati ya timu 12 katika Kundi B ikiwa na pointi 21 huku timu tatu mwishoni zikiwa Stand United yenye pointi 20, Sahare All Stars pointi 19 na Green Warriors pointi 18.

Katika kundi hilo Gwambina inaongoza ikiwa na pointi 40, Geita Gold ikiwa na pointi 30, Mashujaa pointi 26, Gipco, Transit Camp na Arusha FC zikiwa na pointi 25 kila moja na Rhino FC na Pamba FC zikiwa na pointi 22 kila moja.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi