loader
Picha

Kocha Yanga kusajili 4 wa kimataifa

KOCHA Mkuu Yanga SC, Luc Eymael amepania kusajili wachezaji wanne wa kigeni kuimarisha kikosi hicho na kujipanga kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana Luc ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji alisema wachezaji hao ni muhimu kuongeza nguvu na kwenye ripoti yake aliyoiacha alipendekeza wachezaji watoke katika mataifa matatu ambayo ni Ghana, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Nipo Ubeligiji lakini kila kitu niliacha kwa viongozi kwenye ripoti yangu nimetoa mapendekezo ya wachezaji wanne wa kigeni kutoka kwenye mataifa ya Ghana, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa msimu ujao wa ligi,” alisema Eymael.

Alisema kwa msimu ujao kama kocha na benchi la ufundi wamejiwekea malengo ya kuhakikisha wanachukua ubingwa na ili wafanikiwe ni lazima wasajili wachezaji watakaokuwa na nguvu na kuhimili changamoto kwa michezo yote.

Eymael alisema amependekeza majina ya wachezaji kutoka mataifa hayo kwa kuwa wanatumia akili na wana kasi na uzoefu wao utakuwa na tija ndani ya kikosi hicho kwani wataleta changamoto kwa nyota waliopo kwa sasa.

Alisema tangu amejiunga na Yanga amegundua kama anahitaji kuchukua ubingwa ni lazima afanya maandalizi makubwa mapema ikiwa ni pamoja na kuwa na kikosi bora kitakachokuwa na morali kuanzia michezo ya awali ya ligi.

“Tangu nimefika Tanzania nimeiongoza Yanga kwenye michezo kadhaa licha ya baadhi ya viwanja kuwa katika mazingira magumu kwa wachezaji lakini lazima niwe na kikosi kinachoundwa na nyota wenye uwezo binafsi kama Bernard Morisson kwa ajili ya kusaidia kupata matokeo mazuri katika michezo inayoonekana migumu,”alisema Eymael.

Alisema kama wachezaji aliopendekeza atawapata kwa wakati anaamini atatengeneza timu nzuri na wachezaji waliopo huku akibainisha wachezaji wote aliwaachia ratiba ya kufanya mazoezi kulinda viwango vyao.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi