loader
Picha

Kocha: Mazingira kikwazo kwa wachezaji

KOCHA Mkuu wa Mwadui FC, Khalid Adam amesema Tanzania ina wachezaji wenye vipaji vya kucheza soka la kulipwa lakini mazingira yamekuwa kikwazo kwao kuonesha kile walichonacho.

Akizungumza jana Adam alisema ukitoa wachezaji wa Simba na Yanga, klabu zingine wamekuwa wakipambana kucheza kwa kujituma licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki lakini bado hawapewi thamani ili kuongeza morali ya kupambana ili wafike mbali zaidi.

“Mchezaji anayepambana na kutoa mchango mzuri anatakiwa kulindwa na kupewa sapoti ili apate nguvu ya kujituma zaidi lakini wengi Tanzania wanakatishwa tamaa pale wanapokosa vitu muhimu kama watu wa kuwashika mkono ili wafike mbali zaidi” alisema Adam

Adam alitolea mfano kikosi chake cha Mwadui kina wachezaji wa kawaida kama timu zingine lakini wamekuwa wakijituma na kucheza kwa maelekezo hususani kwenye michezo mikubwa na kupata matokeo mazuri.

Alisema ameangalia vizuri michezo ya Ligi Kuu na amegundua wachezaji wengi wanaotoka nje ya nchi wamekuwa na uwezo wa kawaida tena wengine wakizidiwa na wazawa na kuomba viongozi wa klabu kuwapa nafasi wazawa kwani wana uwezo wa kufanya makubwa kama wataaminiwa na kupewa nafasi.

Pia Adam alisema kitendo cha kukosa mfumo rasmi unaojumuisha wataalamu wa kutambua vipaji vya watoto imekuwa changamoto na hata wale wanaonekana kupambana kuonesha kile walichonacho bado hawapewi sapoti ya kutosha.

“Kama nchi tunatakiwa kuwa na mfumo wa kutengeneza kizazi kijacho cha wachezaji ambao watakuwa wanaandaliwa kila hatua, sasa kwa misingi hiyo lazima uwe na wataalamu watakaokuwa makini kuangalia vipaji na kuwaweka pamoja,“ alisema.

Alisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa kutengeneza mfumo kwa kupata wataalamu ambao watakuwa na uwezo wa kuangalia vipaji kwa kuzunguka mikoa yote na kuwaweka kwenye kituo kimoja ambacho kitakuwa na uwezo wakufanya mazoezi pamoja ili kutengeneza timu imara ya taifa.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi