loader
Picha

Coastal- Nondo alitaka kuondoka tukamzuia

UONGOZI wa klabu ya Coastal Union umesisiza haupo tayari kumuachia Bakari Nondo, licha ya kukiri kuanza kupokea ofa kutoka timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizoonesha kuhitaji huduma yake.

Nondo ambaye anacheza nafasi ya beki katika kikosi cha Coastal na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kwa sasa klabu nyingi zinaonekana kupigania kunasa saini yake, hususan Simba na Yanga, wakivutiwa na ubora alionesha kwenye michezo ya ligi pamoja na ile ya timu ya taifa.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Mguto, alisema mchezaji huyo amekuwa nguzo ya Coastal Union, hivyo wataendelea kumlinda, ndiyo maana hawajataka kuweka wazi thamani ya dau lake kwa timu zinazohitaji kumsajili katika msimu ujao.

“Kama mchezaji anahitaji mafanikio kulingana na kazi anayoifanya ikiwamo maslahi kwa kuwa kazi yake anayotegemea ni kucheza mpira, kabla ya msimu huu alitaka kuondoka tukamzuia,”

“Hata sasa hatujafikiria kumuuza, hivyo ni mchezaji wetu halali na yupo ndani ya mipango na mafanikio yetu madogo ya msimu huu,” alisema Mguto Alisema wana taarifa kuwa, kuna timu zinamuhitaji:

“Lakini siyo jambo geni duniani kote kama mtu anafanya vizuri ataonekana na atahitajika, lakini Coastal Union bado hatujafikiria kumuuza.”

Pamoja na msimamo huo wa Mguto, taarifa zinaeleza kuwa, nyota huyo mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu na ameingia kwenye anga za mabingwa watetezi Simba wanaonekana kupania kumpa mkataba ili kuimarisha safu yao ya ulinzi ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi