loader
Picha

Chama Soka Arusha wadaiwa kughushi usajili

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson Maneno, amesema nakala ya cheti cha usajili wa Chama Cha Soka Wilaya Arusha (ADFA) si halali, ni cha kughushi.

Maneno ambaye pia ni Ofisa Michezo Jiji la Arusha, amesema jana kuwa, cheti hicho kilichosajiliwa Aprill 24, 1975 kwa jina la District Football Association (ADFA), atakikabidhi polisi kwa uchunguzi, kwani aliyemkabidhi ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA) Zakharia Mjema.

“Mwaka 1975 kulikuwa na Chama cha Soka Wilaya ya Arusha kilichojulikana kama Football Association Of Tanzania (FAT) ambacho kimesajiliwa kihalali na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini Novemba 13 mwaka 1974 na kupewa namba 611 na nakala ya cheti hicho ninayo ofisini kwangu na hakukuwa na cheti kingine chochote,” alisema.

Maneno alisema inaonyesha viongozi wa ADFA wameghushi cheti na hajui kwa nini waliamua kuchukua hatua hiyo ambayo ni hatari kwa soka la nchi.

Alidai sahihi iliyomo katika cheti hicho ni ya Benson Chacha, Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo nchini na yeye hana muda katika utumishi wa umma kwani yuko kazini kwa muda usizidi miaka minne na ndio maana anasisitiza cheti hicho ni cha kughushi.

“Cheti cha usajili cha ADFA ni feki na kimeghushiwa na viongozi wa chama wanapaswa kujibu mashitaka kwa kufanya hivyo,’’ alisema Maneno.

Alisema alipokuja jijini Arusha miaka minne iliyopita, aliwasiliana na viongozi wa ADFA kutaka kujua uhalali wa chama hicho na kujua usajili wa klabu zote katika wilaya ya Arusha, lakini hakupata ushirikiano wa klabu na kushutumiwa kuvuruga chama kwa kufanya kazi ambayo siyo yake wakati sio kweli.

‘’Viongozi wa ADFA wameidanganya ofisi ya msajili na ofisi zingine za umma, hivyo ni lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo,’’ alisema Mwenyekiti wa ADFA, Omary Walii na katibu wake, Athuman Njiku, walisema hawajui chochote juu ya cheti hicho na hawakuwahi kukabidhiwa walipoingia madarakani na wako tayari kwenda polisi ili waliofanya kitendo hicho waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Walii alisema uongozi wa ADFA haujaghushi cheti hicho na wako tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa Msajili Msaidizi ili wale waliofanya jambo hilo wachukuliwe hatua iwe fundisho kwa wengine wenye kughushi nyaraka za serikali.

“Tuko tayari kutoa ushirikiano kwa Msajili Msaidizi na polisi kwa kumsaka aliyegushi cheti hicho na ADFA sio kichaka cha wahuni kufanya uhalifu hii ni jinai lazima watu wachukuliwe hatua kali, ’’alisema Walii

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: John Mhala,Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi