loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Halmashauri ziige Manispaa Moro kujikinga na corona

MWISHONI mwa wiki iliyopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa maelekezo saba yenye lengo la kudhibiti corona katika vyombo vya usafi ri, majini na nchi kavu.

Maelekezo hayo yanafuatia hatua nyingine kadhaa, ambazo zimechukuliwa na wizara hiyo na serikali kwa ujumla tangu ugonjwa huo ulipoingia nchini.

Tunaipongeza sana serikali kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo.

Pia, tumevutiwa na mikoa mbalimbali kwa kuweka mikakati mbalimbali, kutekeleza maagizo hayo ya serikali ili kujikinga na janga hilo.

Kwa namna ya kipekee, tunaupongeza mkoa wa Morogoro kwa hatua mbalimbali madhubuti, ambazo zimetangazwa na kuanza kuchukuliwa na uongozi wa mkoa.

Kwa mfano mwishoni mwa wiki, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Emmanuele Kalobelo alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Shailla Lukuba kusimamia maagizo mbalimbali kudhibiti corona.

Kalobelo alitoa maagizo hayo, akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, baada ya kutembelea Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, kuangalia utekelezaji wa hatua mbalimbali za kujikinga na corona.

Kwanza, Kalobelo anaitaka Manispaa hiyo kuongeza nguvu ya kutoa elimu endelevu, kusimamia kikamilifu na kuhimiza matumizi ya kunawa mikono kwa sabuni.

Kwamba abiria na wahudumu katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu, wanawe mikono kila mara, hasa abiria kabla ya kuanza safari.

Pia alimwagiza mkurugenzi huyo kuongeza watumishi wa afya katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu ili wafanye kazi kwa zamu.

Hali kadhalika, Manispaa hiyo imetakiwa kuweka vipaza sauti ndani ya stendi hiyo, kwa ajili ya kutoa elimu endelevu kwa wananchi na abiria, kwa vile kituo hicho kina mwingiliano wa watu wengi, wakiwemo wasafiri kutoka mikoa mbalimbali nchini. Elimu hiyo itolewe na wataalam wa afya.

Kwa mujibu wa Katibu tawala huyo, wananchi nao wapunguze msongamano waliouzoea wa kusindikiza ndugu na jamaa zao hadi ndani ya mabasi.

Badala yake, ndugu na jamaa hao, waishie eneo la kusubiria wageni. Kwa wenye mizigo, huduma hiyo ifanywe na wahudumu wa ndani ya stendi tu.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi