loader
Picha

Wazushi bei za vyakula kukiona

SERIKALI imewaonya wafanyabiashara wanaoeneza uvumi kuwa bei za bidhaa vikiwemo vyakula zitapanda kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.

Onyo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Serikali, Prosper Ntahogwamiye, akisema uvumi huo unawafanya watu kuwa na hofu na kununua kiwango kikubwa cha vyakula ili kuwa na akiba wakati maisha yanaendelea kama kawaida.

Tangu Waziri wa Afya nchini humo alipotangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, wananchi wa Bujumbura wamekuwa wakinunua vyakula kwa wingi na kuweka majumbani wakihofu kuwa serikali itaweka zuio la kutotoka nje.

Baadhi ya wafanyabiashara wamechukulia mlipuko huo kama faida kwao kwa kuongeza bei ya bidhaa kama mchele, maharage na mafuta ya kula.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyabiashara wametumia fursa hiyo kupandisha bei ya vyakula, ambapo kilo moja ya maharage aina ya kinure iliyokuwa awali ikiuzwa kwa faranga 1,600, kwa sasa inauzwa kwa faranga 2,300, huku maharage ya njano yaliyokuwa yakiuzwa faranga 2,200 kwa kilo, sasa yanauzwa faranga 2,700.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi