loader
Picha

Kodi ya nyumba yaingiza faranga bilioni 6.7

IDARA ya Usimamizi wa Kodi ya Mapato ya Nyumba katika Mamlaka ya Mapato Burundi, imekusanya faranga za Burundi zaidi ya bilioni 6.7 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020.

Mkuu wa idara hiyo, Joseph Ndayizeye, amesema wamepokea taarifa za watu 6,039 kuanzia Januari mpaka Machi 31, mwaka huu na wanatarajia kuendelea kufanya ukaguzi wa kodi ya nyumba zilizokodishwa.

Amesema mwaka jana, walikusanya faranga bilioni 5. 7 kutoka kwa watu 9,217, wakiwa ni ongezeko la asilimia 14 ikilinganisha na mwaka juzi.

Hata hivyo, amesema idadi ya walipakodi imepungua kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo baadhi ya nyumba kutopangishwa na nyingine kuuzwa.

Kwa mujibu wa sheria ya kodi nchini humo, mwenye nyumba anapaswa kulipa kodi ikiwa nyumba itapangishwa kwa zaidi ya faranga 150, 000.

Aliwataka watu waliochelewa kulipa kodi za pango kulipa mapema iwezekanavyo kabla hawajaanza ukaguzi wa nyumba zote zilizopangishwa na kuwachukulia hatua.

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi