loader
Picha

Wapinga Fufa kupunguza timu Uganda

WIKI kadhaa zilizopita, Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) lilitoa taarifa iliyokuwa na mapendekezo yenye lengo la kuimarisha mashindano nchini.

Taarifa hiyo ilikuwa na mambo machache yaliyojitokeza, lakini kikubwa kilichovuta hisia za wengi hasa wadau wa soka ni pandekezo la kupunguza timu za Ligi Kuu kutoka 16 hadi kufikia 12 katika msimu wa mwaka 2021/22.

Kwa kufanya hivyo, timu sita zitashuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Uganda kuanzia msimu ujao, huku mbili tu zikipandishwa kutoka katika Fufa Big League.

Kwa sasa FA imefanya jambo zuri katika soka la vijana kwa kuanzisha mashindano mbalimbali, ambayo ni Ligi ya Vijana ya Fufa, Odilo, Copa Schools na mengine, ambapo wachezaji wanaofanya vizuri katika mashindano hayo wanapata ajira sehemu fulani.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya kupunguza timu za Ligi Kuu ya Uganda, imepingwa na wadau kadhaa wa soka, akiwemo kipa wa kimataifa wa Uganda Denis Onyango, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Sports Club Villa.

Kipa huyo namba moja wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini nalisema kuwa suala la kupunguza timu katika Ligi Kuu ya Uganda, hilo halikubali kabisa, kwani litapunguza msisimko wa ligi hiyo.

“Kwanza, nafikiri Fufa wangewasiliana na klabu katika hatua ya kwanza kabisa, kitu ambacho hawakukifanya," aliongeza Onyango.

Na watu wengine nao waliotoa mawazo yao walipinga wazo hilo, na kutaka Fufa kubakisha idadi hiyo ya awali au kuongeza ili kongeza msisimko wa ligi hiyo.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi