loader
Picha

Kikapu Arusha yalia uhaba viwanja

CHAMA cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu Mkoa Arusha (ARBA) kimeeleza kukumbwa na uhaba wa viwanja hali inayopelekea kuendesha mashindano kwa changamoto kubwa.

Katibu Mkuu wa ARBA, Phabian Mjarifu alieleza kuwa kiujumla bado suala la viwanja limekuwa tatizo kubwa katika kuhamasisha mchezo huo mkoani Arusha, kwani hivi sasa wamekuwa wakitegemea kiwanja kimoja cha Sheikh Amri Abeid.

"Tatizo la viwanja limekuwa sugu kwa Arusha na hata ligi ya kikapu iliyopita tulitumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambao kiukweli ulikuwa na matumizi mengi, kwani ulihusika pia kwa michuano ya mpira wa miguu, shughuli za mikutano hali iliyopelekea kusimamisha michezo yetu na kufanya ligi kumalizika nje ya muda uliopangwa," alisema.

Alisema tegemeo lao sasa ni kwa mamlaka husika kuliangalia hilo na kusema uwanja wa Ngarenaro ambao ulijengwa na Halmashauri ya jiji la Arusha ukizinduliwa unaweza kupunguza tatizo la viwanja, kwani utatumika na kilio kilichopo kikapungua.

Akizungumzia suala la udhamini alisema bado wanakabiliwa na changamoto kubwa katika uendeshaji wa ligi kwani pia ligi ya kikapu mkoa inajiendesha yenyewe kwa viingilio vya klabu, ambavyo vimekuwa vikitumika kulipa gharama mbalimbali za uendeshaji.

"Pamoja na hayo tunayo mikakati ya kutafuta wafadhili na tayari tumeandikia kampuni kadhaa na baadhi zimeonesha nia ya kutujibu na zingine zimetuelekeza kuzifuata mapema ili ziweze kuona namna gani zitatuunga mkono na hili tutalitekeleza mapema katika ligi ijayo," alisema Mjarifu.

Katika hatua nyingine, ligi ya kikapu mkoa Arusha iliyotarajiwa kuanza kuchezwa mwishoni mwa wiki hii, imeahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona, ambalo lilisababisha Serikali kusitisha shughuli zote zamichezo kwa mwzi mmoja.

Licha ya ukosefu wa viwanja vya kutosha ligi hiyo ilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Timu nane zilitarajiwa kushiriki ligi hiyo ambazo ni Kings, Scorpion, MS-TCDC, Hoopers, Hoo, Polisi Moran, Spider na Palloti.

Timu ya Kings ndio Mabingwa watetezi wa ligi ya kikapu mkoa Arusha, huku timu ya MS-TCDC ikishikilia ubingwa wa Kanda wa mchezo huo.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi