loader
Picha

Beki Pamba atakiwa Coastal Union

MWENYEKITI wa timu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Pamba SC, Aleem Alibhai amethibitisha kuwa mpaka sasa wamepokea mapendekezo ya klabu mbalimbali vya Ligi Kuu, ikiwemo Coastal Union ya Tanga.

Akizungumza na Alibhai amesema tayari klabu ya Coastal Union imependezwa na kiwango cha beki wa kati wa timu yao, Aleco Mwaisaka.

‘’Baadhi ya viongozi wa Coastal Union walinipigia simu na kusema wanamhitaji beki wetu Aleco, hakika ni jambo jema kwetu sisi. Hii si mara ya kwanza mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu kuhitaji wachezaji wetu,’’ Alibhai amesema.

Alisema mpaka sasa timu yao ilishapeleka wachezaji wawili Coastal Union ambao ni Salum Kipemba ambaye ni kiungo mkabaji pamoja na Hassan Kibailo ambaye ni beki wa kulia.

Alibhai amesema katika msimu uliopita waliweza kuwatoa wachezaji wao, Kelvin John na Goodluck Jonathan katika timu ya Ligi Kuu ya Mbeya City.

Kwa upande wake, beki wa timu ya Pamba SC, Aleco Mwaisaka amesema yeye yuko tayari kuchezea timu yoyote kwakuwa mpira ndio maisha yake.

‘’Ni msimu wangu wa nne sasa nacheza Pamba SC lakini kwa sasa najukumu kubwa la kuhakikisha naisaidia timu hii inabakia Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu,’’ amesema Mwaisaka.

Alisema yake kubwa ni kuhakikisha anacheza Ligi Kuu pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi