loader
Picha

Kenya yazuia mitumba kukabili corona

ATHARI za mlipuko wa virusi vya corona imegusa maeneo mengi ya kijamii, ikiwamo mitumba kutoka nje ya nchi kuzuiwa kuingia nchini Kenya.

Ingawa serikali imesema kuwa zuio hilo linalenga kulinda bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwa sababu soko lake limekuwa likiathiriwa na uingiaji wa mitumba ambayo bei yake ni ya chini hivyo kuwavutia watu wengi, lakini baadhi ya maofisa wa serikali wamesema hatua hiyo inalenga zaidi kudhibiti virusi vya corona kuingia nchini humo kutoka nchi nyingine.

Waziri wa Biashara, Betty Maina, aliwaambia waandishi wa habari juzi bila kufafanua kuwa, usalama wa wananchi wa Kenya na uhitaji wa kuimarisha bidhaa za ndani kumesababisha serikali kufikia hatua hii.

“Uingizaji wa mitumba nchini umesitishwa mara moja kwa usalama wa watu wetu na kuzipa kipaumbele bidhaa zinazotengenezwa hapa Kenya kwa kutumia viwanda vyetu,” alisema waziri huyo.

Kwa mujibu wa waziri huyo, kusambaa kwa virusi vya corona ni sababu nyingine iliyochagiza kuzuiwa kwa mitumba kuingia katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki.

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi