loader
Picha

Corona yamzuia kocha Yanga

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael aliyetarajiwa kurejea nchini juzi kuanza kuimarisha kikosi chake, amekwama Ubelgiji kutokana na kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Kutokana na ukubwa wa janga la ugonjwa huo, safari nyingi za ndege zinazotoka moja kwa moja Ulaya kwenda Afrika zimesitishwa na sasa anafikiria kusafiri hadi Ujerumani katika jiji la Frankfurt kuungaunga ndege hadi Misri kisha Ethiopia.

Akizungumza na gazeti hili kutoka Brussels Ubelgiji kwa njia ya mtandao jana, kocha huyo ambaye alikwenda kwao kuoa baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimamishwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Alisema baada ya kushindwa kuondoka juzi kama alivyopanga, sasa anafanya anafanya utaratibu wa kupata tiketi, ingawa anakiri kuwa ni ngumu kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea kuifundisha Yanga.

“Hakuna ndege zinazoingia Ubelgiji kutoka Afrika kwa sasa zote zimezuiliwa kutokana na virusi vya corona na suluhisho langu kwa sasa nitasafiri hadi Ujerumani kwenye mji wa Frankfurt nitachukua ndege zinazoenda Misri kisha nitasafiri hadi Ethiopia na kuunganisha tena ndege hadi Dar es Salaam na safari yangu itadumu kwa wiki moja, ” alisema Eymael.

Kocha huyo, atakapowasili atafikia katika karantini maalumu ya siku 14 kwa gharama zake ili kuangaliwa kama ameambikizwa virusi hivyo vya corona au la na ndipo ataruhusiwa kujiunga na timu yake.

Alisema baada ya kufuata utaratibu huo ambao umepangwa na serikali kitu cha kwanza atakapoingia Yanga atakutana na viongozi wa timu hiyo na kuangalia wachezaji walioongezewa mikataba na kisha kuangalia mapendekezo ya mahitaji ya nyota wapya anaotaka kuwasajili kuimarisha kikosi hicho msimu ujao kama yamefanyiwa kazi.

Eymael alisema mafaili yote ya mahitaji ya msingi ambayo anahitaji kuboresha kikosi hicho alishawaachia viongozi ili kutimiza makubaliano waliyofanya ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa bora zaidi na kutwaa ubingwa msimu ujao.

“Nawaamini viongozi pamoja na mdhamini GSM, yote yataenda sawa na nikifika lazima tufanye kikao cha mrejesho wakati tunasubiri taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu ratiba ya kumalizia michezo iliyosalia ya Ligi,” alisema.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 nyuma ya vinara Simba wenye pointi 71 na Azam FC waliopo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 54.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi