loader
Picha

Gor Mahia kupewa ubingwa

RAIS wa Shirikisho la Kenya (FKF), Nick Mwendwa amesema kuwa Gor Mahia itatangazwa bingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu huu endapo ligi haitaendelea tena kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Ugonjwa huo hadi sasa umegharimu maisha ya watu sita nchini hapa huku ikirekodi waathirika 142 wa janga hilo.

Kwa mujibu wa mtawala wa soka la vijana, matokeo yote ya timu zote hadi sasa msimu huu, ndio yatatumika kuamua nani bingwa na timu zipi ambazo zitashuja daraja.

Akizungumza katika stesheni ya redio ya hapa mwishoni mwa wiki, Mwendwa alisema sheria za Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) zitatumika endapo msimu hautakamilika na hali ndivyo itakavyokuwa kwa Ligi Kuu ya Kenya.

“Ikiwa ligi itasimama kabla ya nusu ya msimu kumalizika katika haitamalizika kabla ya nusu ya msimu katika mazingira yoyote ligi ikafutwa kwa muda usiojulikana. Endapo mechi zimechezwa zaidi ya nusu na chini ya asilimia 75 msimamo huo ndio utatumika kuamua mshindi kwa kuangalia msimamo wa wakati ule,“ alisema Mwendwa.

Hatua nyingine itakayotumika ni msimu huu tangu kati ya mechi 10 na 11 zilizobaki itategemea na kila timu ambayo haitafikia asimilia 75.

Hii ina maana kuwa kwa njia yoyote kama ligi haitaendelea kutokana na mlipuko huu wa corona, K’Ogalo ndio watakuwa mabingwa na kulitwaa taji hilo kwa msimu wan ne mfululizo.

Baada ya kuchezwa raundi 16 za mechi za ligi, Gor Mahia ina pointi 38, nne juu ya Tusker iliyopo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 34, ikifuatiwa na Kakamega Homeboyz yenye pointi 33.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi