loader
Picha

Simba- Ligi imalizike uwanjani

UONGOZI wa Simba umesisitiza kuwa lazima ligi imalizike kwa kuchezwa uwanjani na kumpata bingwa halali na sio kumalizwa mapema baada ya kusimama kutokana na sababu ya virusi vya corona.

Tayari klabu kadhaa zilijitokeza na kutaka msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizwa mapema, kwani hawajui katazo la michezo litamalizika lini kutokana na virusi vya corona.

Kauli hiyo ya Simba imekuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiriki ligi hiyo kutoa maoni ya kuomba ligi hiyo ifutwe licha ya kusalia michezo 10 kumalizika.

Licha ya timu ya Simba kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa vinara kwa pointi 71 na kutengeneza utofauti wa pointi 17 na Azam FC, wanashika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi 54 bado uongozi wao unaamini ligi imalizikie uwanjani.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza amesema kabla ya kuchukua uamuzi lazima kwanza kuangalia hali ya Tanzania na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huo, ndio nini kifanyike.

“Lazima tuchukue maamuzi tukiangalia hali yetu Tanzania, tuache uongozi kutoka serikalini ufanye kazi yake na kufanya maamuzi kulingana na kile tunachosoma na kuona kinachotokea katika mataifa mengine, lakini ni matakwa yangu ni vema ligi ikamalizika uwanjani, lakini kama ikishindikana basi maisha ni muhimu zaidi kuliko soka,“alisema Mazingiza.

Alisema itakuwa mapema kuamua ligi ifutwe kabla ya mwezi huu na kwa maamuzi ya njia yoyote watakayoenda kutolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB), basi yatatakiwa kuzingatia tija na maslahi ya maendeleo ya mchezo huo nchni.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi