loader
Picha

Corona kuathiri mikataba ya wachezaji Rwanda

IKIWA janga la mlipuko wa virusi vya corona halitamalizika hadi ifi kapo Mei 31 mwaka huu, Rayon Sports itakuwa moja ya klabu zitakazoathirika zaidi kutokana na wachezaji wake wanne kumaliza mikataba yao.

Beki wa kulia wa Rayon Sports, Eric Radu Iradukunda, viungo, Ally Niyonzima na Fabrice Mugheni Kakule na msham- buliaji Michael Sarpong watakuwa nje ya mikataba yao ifikapo Mei 31, 2020.

Kawaida klabu za Ligi Kuu ya Rwanda zinasaini wachezaji wake hadi Julai 4 wakati wa fainali ya Kombe la Amani inachezwa lakini wachezaji wengine mikataba yao inamalizika Mei 31, wakati ligi inapomalizika.

Nini kitatokea kwa wachezaji ikiwa mikataba yao itamal- izika kabla ya kumalizika kwa ligi? Wakati ligi ikisimama Machi 24, 2020, mechi nyingi zilikuwa zimechezwa na kubaki sita tu labla ya kukamilika kwa ligi hiyo yenye timu 16.

Awali, msimu huo wa ligi ulitarajiwa kukamilika Mei 21, lakini hadi sasa viongozi hawana uhakika lini itamalizika baada ya kuibuka kwa janga hilo.

Hatahivyo, imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) liko katika mazungumzo na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) na Fifa kupata ruhusu maalumu ya mkataba wa muda mfupi wa wiki kwa wiki kwa wale wachezaji walio huru.

Ligi Kuu ya Rwanda na shughuli zingine za michezo zimesimamishwa kuanzia Machi 15, 2020 wakati serikali ikitoa hatua ya kupambana na mlipuko wa virusi vya corona.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi