loader
Picha

Licha ya corona Ligi Kuu Burundi yaendelea

WAKATI nchi nyingi duniani zikisimamisha shughuli zao za michezo ili kukwepa mikusanyiko inayoweza kusababisha kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona, Ligi Kuu ya Burundi inaendelea.

Uamuzi huo ulifikiwa juzi Jumapili katika kikao cha Shirikisho la Soka la Burundi na klabu za Ligi Kuu licha ya kuwepo kwa tishio la kuenea kwa virusi vya corona.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni moja kati ya nne duniani, ambazo ligi zao za soka zinaendelea baada ya shughuli nyingi za michezo, ukiwemo wa soka kusimamishwa kutokana na janga la corona, ambalo linaisakama dunia.

“Baada ya kuwasiliana na Waziri wa Afya, Thaddeus Ndikumana, mkutano mkuu uliamua kuwa mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza na Pili yaendelee wakati wakiangalia hatua nyingine ya kuchukua,

“lilisema shirikisho hilo katika taarifa yake baada ya kikao hicho, ambacho kilikuwa kikiangalia kama ligi hiyo iendee au la.

Ziko kesi tatu zilizothibitishwa za maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini Burundi, ambayo pamoja na za Belarus, Nicaragua na Tadjikistan ndizo pekee ligi zao za soka zinaendelea kuchezwa.

Msimu wa soka nchini Burundi, ambao timu yao ya taifa mwaka jana ilicheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) nchini Misri, umebakisha raundi tatu tu kabla ya kukamilika kwake.

Ukiiondoa Burundi, nchi nyingine zote zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki zimesimamisha ligi zao kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.

MSANII Faustina Charles ‘Nandy’ siku ya harusi na mchumba William ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA, Burundi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi