loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajanja ‘waichapa’ Marekani barakoa milioni 36

JUMUIYA yenye nguvu kubwa jijini California iliyotafuta barakoa milioni 39 kwa ajili ya watumishi wa afya wanaopambana na janga la virusi vya corona, imejikuta ikiingia katika kashifa , baada ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kubaini kutokuwepo kwa barakoa zilizozungumzwa.

Wakili wa Pennsylvania, Scott Brady alisema maofisa wa FBI na waendesha mashtaka walikutana na sakata hilo, wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta barakoa kwa ajili ya Wakala wa Masuala ya Dharura.

Brady alisema wapelelezi hao waliunganisha tukio hilo na mfanyabiashara kutoka Pittsburgh ambaye alidai kuwa amekuwa akishirikiana na jumuiya hiyo kupata mamilioni ya barakoa ambazo baadhi yake zilihifadhiwa kwenye ghala huko Georgia.

Brady alisema mfanyabiashara huyo amekuwa akitumia WhatsApp kuungana na dalali wa huko Australia na muuzaji kutoka Kuwait, ambao wote sasa wanatafutwa na FBI.

Alisema jumuiya hiyo na mfanyabiashara aliyekataa kumtaja jina, wanaonekana kuwa ni watu wa kati ya dili hilo ambao nao pia wamedanganywa. Ahadi ya barakoa milioni 39 ilitolewa kwa mara ya kwanza Machi 26 pale Jumuiya ya Kimataifa ya Waajiri na Umoja wa Watoa Huduma za Afya kutangaza kuwa imepata barakoa hizo ndani ya saa 48 baada ya kuhangaika kutafuta mtu wa kuwasambazia. Kupatikana kwa barakoa hizo kuliripotiwa na vyombo vya habari na kuandikwa kwa orodha ya hospitali na wakala watakaozinunua. Katika mtandao wake wa Facebook kiongozi wa Jumuiya hiyo Dave Regan alidai tayari barakoa hizo zimeshanunuliwa na wafanyakazi watazipokea muda si mrefu. Baadhi ya hospitali, vituo vya afya na wakala mbalimbali walianza kutoa oda zao za kununua barakoa hizo na hospitali ambazo hazikuweka oda ziliumbuliwa na kusimangwa kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, baada ya muda taasisi zilizoweka oda za kununua barakoa hizo zilianza kuingiwa na wasiwasi baada ya kukosa taarifa za mahali mzigo ulikofikia na wapi pa kuuchukulia. Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo wa Pittsburgh alikubaliana na wanaomuuzia kununua barakoa moja kwa dola za Marekani 3.50 huku jumuiya hiyo ikinunua barakoa moja kwa dola za Marekani tan

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na ...

foto
Mwandishi: SACRAMENTO, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi