loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Utengenezaji, utumiaji barakoa muhimu kuzuia corona

SERIKALI imesema wataalamu wa afya, wanamalizia kufanya mchakato wa namna bora na sahihi ya kutengeneza barakoa zinazofaa kuvaliwa na wananchi, kama njia mojawapo ya kujikinga na virusi vya corona.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amesema wataalamu wataalamu watakapokamilisha mchakato huo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu atatoa maelekezo kwa wananchi jinsi ya kuzitengeneza.

Dk Ndugulile amesema barakoa zinazotengenezwa kwa vitambaa vya nguo, ndizo zitatolewa maelekezo ya jinsi ya kuzitengeneza ili wananchi waweze kuzitumia, kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya corona na kufuata maelekezo mengine ya jinsi ya kujikinga.

Amesema kwa sasa wataalamu wanakamilisha mchakato wa kuandaa maelekezo ya namna sahihi ili ziweze kufaa, bila kusababisha athari zozote kwa watumiaji.

Pamoja na faida nyingine, Naibu Waziri alisema hatua hiyo itasaidia mtu akipiga chafya kama amevaa barakoa, majimaji yatabakia ndani yake au akikohoa, virusi havitaweza kuruka na kumpata mtu mwingine, hivyo kusaidia kupunguza maambukizi.

Kwa dhati kabisa tunaipongeza serikali, kwa kuendelea kubuni mikakati mbalimbali, yenye lengo la kupunguza maambukizi ya corona kwa jamii yetu.

Ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa maambukizi yanaweza kusababishwa na hewa, kutokana na virusi kuwa na uwezo wa kukaa hewani kwa saa kadhaa, ni wazi kuwa matumizi ya barakoa katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu, hayatakwepeka.

Kama ndivyo, ni jambo la kuipongeza serikali kwa kuona umuhimu na ulazima wa kuwafundisha wananchi namna nzuri na sahihi ya kutengeneza barakoa ili itakapolazimika wananchi kuanza kuzitumia, wanapotoka majumbani kwenda sehemu mbalimbali, basi upatikanaji wake uwe rahisi kwa wananchi wenyewe kuzitengeneza kwa usahihi.

Tunafahamu fika kuwa vifaa vya kujikinga na corona, vimekuwa adimu au vimepanda bei tangu maambukizi yaliporipotiwa kuingia nchini, hivyo njia ya kuwafundisha wananchi kutengeneza barakoa kwa kutumia vitambaa, itasaidia upatikanaji kuwa rahisi lakini pia gharama kuwa nafuu.

Ni imani yetu kuwa baada ya maelezo hayo ya awali ya Naibu Waziri Ndugulile na wakati ambapo tunaendelea kusubiri maelekezo ya Waziri Ummy, wananchi wataendelea kujiweka tayari kupokea maelekezo hayo kwa njia sahihi, bila kupotosha kile kitakachoelekezwa.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi