loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera wadau, sasa tujifunge vibwebwe kuimaliza corona

JANA wadau wa maendeleo nchini wametoa misaada mbalimbali kwa Serikali yenye thamani ya Sh bilioni 3.2 ikiwa ni mchango wao katika mapambano dhidi ya ugonjwa homa kali ya mapafu (Covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona.

Misaada hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Tumeelezwa kuwa fedha taslimu iliyowasilishwa kwa mfano wa hundi kiasi cha Sh bilioni 3.185 , pia kuna vifaa kinga mbalimbali vya kujikinga na corona vyenye thamani ya Sh milioni 15.

Pamoja na kuwapongeza wadau hao wa maendeleo, tunaamini kwa msaada huo utaongeza nguvu kwa Serikali katika juhudi zake za kuhakikisha kwamba kila kitu kipo sawa katika mapambano dhidi ya corona.

Ni dhahiri kwamba wadau hao wa maendeleo wameonesha uzalendo wao ili kusaidia serikali kuwa na uwezo wa ziada katika kukabiliana na adui corona.

Pamoja na kusifu taasisi za San & Lam, Faida Letshego Bank, Financil Secto Depending Trust (FSDT), TUICO-Taifa, Kampuni ya huduma za simu ya Vodacom, Kampuni ya Songas, Kampuni ya Yepi Merkedzi, Benki ya NBC pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa uzalendo wao, tunapenda kila mtanzania kwa nafasi yake kuiga mfano huo.

Aidha tunapenda kuwaomba wananchi, kutambua kwamba taifa kwa sasa lipo katika vita dhidi ya ugonjwa huu ni vyema wakaonesha heshima ya michango ya aina hii kwa kufuata maelekezo yanayotolewa ya namna ya kujihami na kuwepa maambukizo.

Hali hiyo inaweza kukabiliwa kwa kuzingatia kanuni za afya za kujikinga na ugonjwa huo sambamba na kufuatilia maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi ya Covid-19 ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka.

Tunasisitiza pamoja na njia hizo inafaa Watanzania wasisubiri serikali kutumia nguvu kidogo katika vita dhidi ya corona kwa kutambua wenyewe kwamba misongamano na mikusanyiko iwe katika usafiri au katika kazi si sahihi kwa wakati huu na huu si mzaha.

Lakini pia tunasema kwamba wale wenye kujihisi kuwa na dalili za ugonjwa wa corona wasibaki nyumbani bali wawahi hospitali kwanza kwa usalama wao pia na usalama wa wapendwa wao.

Pamoja na hatua zote hizo tusisahau kumuomba Mungu atunusuru na ugonjwa huu wa corona, Amina.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi