loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuzingatie maagizo ya Serikali, wataalamu kudhibiti corona

Tangu ugonjwa wa corona ulipozuka, kumekuwa na maagizo mbalimbali, yanayotolewa kila siku kwa wananchi, juu ya namna ya kukabiliana nao.

Hivyo, Kwanza tunapongeza viongozi wa juu wa kitaifa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee na wataalamu wa afya, kwa kutoa maagizo na maelekezo hayo mara kwa mara ya kuzingatia kwa wakati huu.

Kwa mfano, wananchi wanahimizwa kuzingatia namna bora ya kujenga afya ya kimwili na kiakili, kwa kuepuka wasiwasi uliopitiliza, kwa kuwa wasiwasi una athari katika mfumo wa kinga ya mwili.

Hilo ni jambo muhimu mno kwa kuwa wakati huu, kwani baadhi ya watu wamekuwa wakitoa taarifa potofu, zinazoharibu afya ya akili na kuwaingiza watu kwenye msongo, taharuki na wasiwasi uliopitiliza.

Mtaalamu wa utoaji elimu ya juu ya corona kutoka Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma cha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Tumaini Haonga anafafanua kuwa kudhoofu au kuimarika kwa mwili wa mtu mwenye virusi, kunategemea uimara wa kinga ya mwili.

Haonga anasema msongo wa mawazo na hali ya wasiwasi uliopitiliza, vinasababisha kinga ya mwili kushuka, hivyo mtu akipata maambukizi, kuna hatari ya kudhoofu zaidi kuliko watu wengine.

Kwa mujibu wa Haonga, jambo la msingi katika kipindi hiki, ni kila mtu ajitahidi kufuata taarifa rasmi; na kutambua kwamba ingawa vipo vifo vinavyoripotiwa, lakini bado kuna watu wanapona.

Ukiangalia uwiano wa wanaofariki na kupona, wanaopona ni wengi hivyo tukiweka nguvu katika tahadhari na kuwahi kupata tiba, watu wengi watapona.

Pili, tunalipongeza Shirika la Afya Duniani (WHO) linavyojitahidi kutoa maelekezo kila mara ya jinsi ya kupambana na ugonjwa huo hatari duniani.

Kwa mfano, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedross Ghebreyesus kupitia video fupi hivi karibuni anataja baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati huu, kama vile mtu anapohisi ana msongo wa akili, kuchanganyikiwa na hofu.

Anasema mtu anapohisi ana hofu au msongo wa mawazo, aongee na watu anaowafahamu na anaowaamini, asikilize muziki, kusoma vitabu na kucheza michezo. Anashauri kuwa mtu asijaribu kusoma au kuangalia habari nyingi, endapo habari hizo zinamfanya ahamaki.

Kwa ujumla, kinachotakiwa wakati huu ni kuzingatia kikamilifu maagizo na maelezo ya serikali na wataalam katika kupambana na ugonjwa huo hatari.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi