loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DK ELISHA AACHE KURUKA KIMANGA

TUMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa iliyoandikwa na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Elisha Osati, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ambako amekanusha habari iliyochapishwa na gazeti hili toleo namba 4754 la Ijumaa Aprili 24, mwaka huu ukurasa wa 4, yenye kichwa cha habari ‘Madaktari waridhishwa na upatikaji wa vifaa vya kazi.’

Kupitia akaunti yake ya Twitter Dk Elisha ameandika; ‘Kauli ya gazeti la HabariLeo ya Madaktari kuridhishwa na upatikanaji wa vifaa kinga si za kweli, naomba ieleweke mpaka sasa bado vifaa kinga ndio kilio chetu watoa huduma za afya. Tunaomba serikali & wadau waendelee kusaidia upatikanaji wa vifaa. Tunawashukuru wote wanaoendelea kujitoa.’

Kwa bahati mbaya, kanusho hilo la Dk Elisha dhidi ya habari iliyochapishwa na gazeti hili imesambazwa katika maeneo mbalimbali hususani katika mitandao ya kijamii, ambapo wanaolisambaza akiwemo Dk Elisha mwenyewe wanajaribu kutaka kuiaminisha jamii kuwa habari hiyo ni ya uongo, jambo ambalo si sahihi.

Ukweli ni kwamba; yote yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni yale yaliyoelezwa na Dk Elisha wakati wa mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu Aprili 23, mwaka huu.

Kwa bahati nzuri sana mazungumzo baina ya Dk Elisha na gazeti hili yalifanywa kwa njia ya simu, na kwa bahati nzuri zaidi kumbukumbu ya mazungumzo ya simu haipotei na inaweza kupatikana wakati wowote inapohitajika.

Uongozi wa gazeti hili unasisitiza kwamba kilichoandikwa kilizingatia misingi ya maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari ya ukweli na usahihi.

Dk Elisha kama kiongozi wa madaktari na mtu mwenye dhamana na heshima kubwa katika jamii, anapaswa kusimamia kile anachokiamini na kukisema bila kujali shinikizo la aina yoyote; kwani ni kweli kuwa zipo jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo kununua na kusambaza vifaa vya kazi.

Hata hivyo mbali na juhudi hizo haimaanishi kwamba tatizo la uhaba wa vifaa kwa watoa huduma za Afya limetatuliwa kabisa.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi