loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tudumishe Muungano kwa maslahi ya wengi

JANA Watanzania waliadhimisha miaka 56 ya Muungano huku viongozi wakiomba udumishwe kwa maslahi ya wananchi wenyewe.

Kuadhimisha siku hii, Rais John Magufuli amesamehe wafungwa 3,973 waliokuwa wakikabiliwa na makosa mbalimbali huku akiwapunguzia adhabu ya kifo baadhi yao.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye wizara inayohusika na masuala ya Muungano iko chini yake, amewataka wananchi kuudumisha kwani una manufaa kwa wote.

Aidha, Waziri mwenye dhamana na Muungano, Mussa Azzan Zungu naye akasisitiza umuhimu wa Muungano kwa nchi kikanda na kimataifa.

Kama ilivyo viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT), viongozi wa Zanzibar wakiongozwa na Rais Ali Mohamed Shein, nao wamezungumzia umuhimu wake.

Tunaungana na viongozi hao wote na wananchi wa pande zote mbili za Muungano kupongeza maono ya viongozi waasisi wa nchi, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume kuunganisha nchi.

Muungano ni matokeo ya viongozi hao kwa nia njema ya kujenga umoja, mshikamano wa watu wao, kushirikiana kijamii, ulinzi na usalama, uchumi, waliunganisha nchi zao kuwa moja.

Ni kwa sababu hiyo Watanzania wanaporejea kumbukizi ya muungano huo Aprili 26 ya kila mwaka kuwaenzi kwa kuwa mfano wa viongozi waliojitoa nafasi zao kwa maslahi ya wengi.

Kitendo cha kukubaliana kuunganisha nchi zao kiliweka msingi wa usalama mkubwa wa nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii uliopo sasa na unazidi kuendelezwa na serikali zote mbili.

Ni kwa msingi huo tunasema, pamoja na nchi sasa kuwa kwenye janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19, ni muhimu wakauenzi muungano kwa vitendo.

Muungano huo unabaki kama alama kubwa ya umoja, upendo, mshikamano kati ya watu wa visiwa vya Unguja na Pemba na pia iliyokuwa Tanganyika uliosimikwa katika udugu wa damu.

Kwamba watu wa pande mbili za muungano kwa miaka nenda rudi wamekuwa wakioleana ni ushahidi wa jinsi muungano huu ulivyoshibana.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi