loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaoingia kwa njia za ‘panya’ kuwekwa karantini

MAMLAKA za kaunti ya Yei River zimeanzisha eneo maalum kwa ajili ya kuwatenga wasafi ri wanaoingia Sudan Kusini kwa njia zisizo rasmi kutoka nchi jirani, ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kituo hicho kipo katika eneo la Ronyi Payam katika barabara ya Yei-Kaya. Ofisa Utawala wa jimbo hilo, Felix Amule, alisema katika eneo hilo kumekuwa na muingiliano mkubwa wa watu, baadhi wakitumia njia za panya kuingia Yei kutoka nchi jirani za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alisema kituo hicho kitatumika kuwaweka karantini washukiwa watakaokamatwa na askari wa ulinzi na usalama kwa kuingia kinyume cha utaratibu nchini humo kupitia Yei.

“Watu watakaoingia kinyume cha sheria watawekwa katika karantini mpaka itakapohakikishwa usalama wao kiafya kabla ya kuruhusiwa kuchangamana na familia zao na jamii kwa kuwa wametoka kwenye nchi zenye maambukizi,” alisema Amule.

Alishauri wananchi kuepuka wasafiri haramu wanaokiuka taratibu za usalama wa afya, kwani watakaokamatwa watafikishwa mahakamani.

foto
Mwandishi: YEI RIVER

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi