loader
Picha

Marekani kutoa dola milioni 13 kupambana na corona

MAREKANI imetangaza kutoa dola za Marekani milioni 13.1 kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, nchini Sudan Kusini.

Aprili 16, mwaka huu, Marekani ilitangaza kutoa dola za Marekani milioni 5.1, ikiwa ni nyongeza ya dola milioni nane ilizoahidi Machi 27, mwaka huu. Taarifa ya Balozi wa Marekani nchini hapa, Tom Hushek, ilieleza juzi kuwa, nchi hiyo katika misaada yake ya afya na ya kibinadamu kwa Sudan Kusini, inaelekeza kupambana na magonjwa ya ebola, ukimwi, kifua kikuu, malaria na corona.

Alisema kati ya fedha hizo, dola milioni 11.5 kutoka Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni kwa ajili ya kukabiliana na majanga na dola milioni 1.6 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kusaidia kukabiliana na corona kwa wakimbizi nchini humo.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: JUBA

1 Comments

  • avatar
    Jackson salumu
    28/04/2020

    Imefanya jambo jema sana kutoa msaada huo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi