loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tutaishinda corona kwa kujihadhari na si kujifungia

SIKU chache baada ya Rais John Magufuli kueleza msimamo wa serikali kuwa haina mpango wa kuifunga Dar es Salaam wala mkoa mwingine wowote, kama njia za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, wataalamu mbalimbali wameunga mkono hatua hiyo.

Rais Magufuli kwa upendo wa pekee na wa aina yake dhidi ya raia wake, amejaribu kueleza mbinu ambazo wananchi wake wanaweza kujiepusha na maambukizi ya virusi hivyo hatari na Taifa likabaki salama siku au miezi michache baadaye.

Siku kadhaa baada ya Rais kusisitiza umuhimu wa wananchi, kutumia mbinu mbalimbali kujiokoa na kadhia hii ya coona na si kujifungia ndani, wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya, uchumi na jamii wameunga mkono maelekezo hayo ya Rais Magufuli.

Mathalani, wataalamu hao wamesema katika kupambana na janga la virusi vya corona, ni vyema wananchi wa kawaida wakashirikishwa kuchagua njia bora za kukabiliana nazo, badala ya kulazimisha kuweka amri ya kutotoka kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa kuliko ugonjwa wenyewe.

Kwa mfano, Mkurugenzi wa Taasisi ya Amani Duniani, Profesa Alex de Waal ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tufts cha nchini Marekani na mwandishi wa vitabu mbalimbali mashuhuri, ameshauri kuwa katika kukabiliana na janga la corona, si kila mbinu inaweza kuwa muafaka ikiwemo ya katazo la watu kutoka nje.

Kwa dhati kabisa tunaendelea kuunga mkono msimamo wa serikali wa kuendelea kuwaelekeza wananchi mbinu mbalimbali za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona bila kulazimika kuifunga nchi, kwani kama alivyosema yeye mwenyewe na wanavyoendelea kusema wataalamu mbalimbali duniani, madhara ya kuwafungia ndani raia ni makubwa zaidi kuliko hata corona yenyewe.

Katika nchi za Dunia ya Tatu ambazo nyingi zipo katika Bara la Afrika, zuio la wananchi kutoka majumbani, linaweza kuleta athari kubwa sana ikiwemo kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa watu kufa kwa njaa, kutokana na ukweli kuwa uwezo wa kiuchumi wa mataifa hayo na wananchi wake ni mdogo sana.

Ni kutokana na sababu hizo, ndio maana tunashawishika kuieleza jamii kuwa tutaishinda corona kwa kuchukua hatua mbalimbali za tahadhari, kama alivyotushauri Rais wetu mpendwa na si kwa kujifungia ndani na kuacha kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi